Skip to content

Tamko la Imani

Tunaamini katika:

  1. Mungu mmoja wa kweli anayeishi milele katika nafsi tatu-Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
  2. Upendo, neema na ukuu wa Mungu katika kuumba, kudumisha, kutawala, kukomboa na kuhukumu ulimwengu.
  3. Uvuvio wa kiungu na mamlaka kuu ya Maandiko ya Agano la Kale na Jipya, ambayo ni Neno la Mungu lililoandikwa—linaloaminika kikamilifu kwa imani na mwenendo.
  4. Heshima ya watu wote, waliofanywa mwanamume na mwanamke kwa mfano wa Mungu ili wapende, wawe watakatifu na wajali uumbaji, lakini wameharibiwa na dhambi, ambayo huleta ghadhabu ya kimungu na hukumu.
  5. Umwilisho wa Mwana wa milele wa Mungu, Bwana Yesu Kristo—aliyezaliwa na bikira Maria; kweli kweli Mungu na binadamu kweli kweli, lakini asiye na dhambi.
  6. Dhabihu ya upatanisho ya Kristo msalabani: kufa badala yetu, kulipa gharama ya dhambi na kuushinda uovu, hivyo kutupatanisha na Mungu.
  7. Ufufuo katika mwili kwa Kristo, matunda ya kwanza ya ufufuo wetu; kupaa kwake kwa Baba, na utawala wake na upatanishi wake kama Mwokozi pekee wa ulimwengu.
  8. Kuhesabiwa haki kwa wenye dhambi kwa neema ya Mungu pekee kwa njia ya imani katika Kristo.
  9. Huduma ya Mungu Roho Mtakatifu, anayetuongoza kwenye toba, hutuunganisha na Kristo kupitia kuzaliwa upya, hutia nguvu ufuasi wetu na kuwezesha ushuhuda wetu.
  10. Kanisa, mwili wa Kristo wa mahali pamoja na wa ulimwengu wote, ukuhani wa waamini wote—uliopewa uzima na Roho na kupewa karama za Roho ili kumwabudu Mungu na kutangaza injili, kukuza haki na upendo.
  11. Kurudi binafsi na kwa kuonekana kwa Yesu Kristo ili kutimiza makusudi ya Mungu, ambaye atawainua watu wote kwaajili ya hukumu, kuleta uzima wa milele kwa waliokombolewa na hukumu ya milele kwa waliopotea, na kuanzisha mbingu mpya na dunia mpya.