Skip to content

Maadili ya msingi

Msingi wetu ni Kristo na Utatu wa Mungu

Al Massira inaamini katika Mungu ambaye ni ushirika wa – Baba, Mwana na Roho Mtakatifu – ambaye amefunuliwa mara kwa mara kupitia Maandiko yote. Mungu wa Utatu alijidhihirisha kupitia Yesu Kristo ambaye ndiye jiwe kuu la pembeni. Yeye ndiye mwanzo na mwisho; njia, kweli na uzima. Al Massira imejidhatiti katika kuwa mwaminifu katika kweli hizi mbili, jinsi inavyowasilisha ujumbe wa Biblia na jinsi inavyowawezesha na kuwafuasa watu katika huduma.

Maadili yote ya msingi yafuatayo yanapata chanzo chaoke katika Adili hili la kwanza na muhimu zaidi.

Tunatoa sauti mpya

Hakuna nyenzo nyingine ya kisasa, ambayo tunaifahamu, ambayo inawasilisha Habari Njema ya Yesu kutoka katika utamaduni wa Mashariki ya Kati. Kwa maana hii Al Massira ni “sauti mpya”. Al Massira iliibuka kujibu maswali ya waumini kutoka asili ya Mashariki ya Kati wakipambana na maswali yale yale ya kitheolojia ambayo ulimwengu wa Kiislamu umekuwa ukipambana nayo kwa miaka 1400. Wakati watu kutokea kwenye chimbuko lolote, ambao wameumbwa kwa sura yake, wanapokuwa wafuasi wa Masihi, watagundua jukumu la pekee, walilopewa na Mungu la kumfunua Masihi na kazi Yake kwa mataifa yote.

Tunafanya kazi kwa ushirikiano

Mungu wa Utatu wa Biblia ni ushirikiano wa karibu na wenye muunganisho wa kina. Tangu mwanzo, Al Massira, imekuwa ushirikiano wa Wakristo kutoka asili tofauti za kikabila, kitamaduni na madhehebu. Tunajaribu kuakisi kipengele hiki cha asili ya Mungu katika ushirika na kazi yetu. Jukwaa la umoja limejengwa katika jukumu la kutimiza ‘Agizo Kuu’ kwa watu wengi zaidi ambao hawajafikiwa duniani – pia ni mahali ambapo utofauti unakaribishwa na kusherehekewa. Jukwaa hili ni mahali ambapo watu wanaweza kuchangia wakati wao, zawadi na uwezo wao kutimiza maono na utume wa Al Massira. Al Massira inalenga kuhimiza muundo huu wa ushirikiano katika kila ngazi ya uendeshaji wake.

Sisi ni wa uhusiano na wa mwili

Bwana wetu ni uhusiano na amechagua, kama njia yake kuu ya ufunuo, kuja katika mwili. Pia ametualika tuje kuwa familia pamoja na familia yake. Tumeitwa kufanya wafuasi wa mataifa yote ambayo huanza na uinjilisti na kuendelea katika njia ya wokovu hadi katika kukomaa na kuwajenga waamini katika kanisa na katika kusudi ambalo Mungu ametuumba kwa ajili yake. Tunaamini kuwa uhusiano ndio njia bora zaidi ya ufuasi na Al Massira hufanya kazi vyema katika muktadha huu. Ni muhimu kujenga uhusiano na wale tunaowaandaa ili tuweze kutiana moyo kwa shuhuda za kile ambacho Mungu anafanya. Tunawahimiza watu kutumia rasilimali na mbinu ya Al Massira katika muktadha wa uhusiano na jumuiya kwani hii inatoa fursa asilia kwa mahusiano kukua na kwa vikundi kukua na kuwa vikundi vya ufuasi ambavyo vinaweza baadaye na kwa kawaida kusababisha ukuaji wa kanisa na kulizidisha.

Tunajenga nyumba mpya

Al Massira imejikita kufichua ujumbe wa Biblia na kile ambacho Wakristo wanaamini kweli. Tunafanya hivi kwa ujenzi wa nyumba mpya kutoka msingi kwenda juu – kuonyesha ujenzi na uthabiti wa ufunuo wa Mungu. Al Massira inatumia biblia na mpangilio wa masimulizi kufichua Utu na kazi ya Kristo na asili ya Mungu kama inavyofunuliwa katika Agano la Kale na Jipya. Al Massira inachunguza hadithi, ishara na unabii wa Agano la Kale ili kuonyesha asili thabiti ya ujumbe. Al Massira inajaribu kutoharibu mifumo mingine ya imani wala kutafsiri upya imani ya Kikristo kutoka katika mfumo mwingine wa ki-imani. Kwa hiyo hatutumii maandiko mengine ya kidini, wala haturejelei watu wengine muhimu wa kidini. Ulinganisho kati ya maandiko/wahusika wa Biblia na maandishi na wahusika wengine wa kidini pia haujachunguzwa.

Tunaunda nafasi salama na wazi

Al Massira anahimiza kuundwa kwa mahali salama ambapo marafiki wanaweza kushiriki maoni yao na kufurahia majadiliano ya wazi bila kuwekwa chini ya shinikizo kwa wote kukubaliana au kukubali mtazamo fulani. Kusimulia hadithi na kuuliza maswali kunahimizwa pamoja na uchunguzi wa Biblia nzima ukitoa nafasi kwa Roho Mtakatifu kufichua ukweli na kuchochea jibu lolote. Washiriki wa kikundi cha Al Massira pia wanahimizwa kusimulia hadithi tena na kushirikisha nyenzo ndani ya vikundi vyao vya kijamii na familia.