Skip to content

Jiunge na kikundi

Njoo ujionee mwenyewe Al Massira. Ikiwa una hamu ya kujifunza juu ya mpango wa Mungu wa wokovu na kusudi lake kwa maisha yako kupitia macho ya manabii kutoka kwa Adamu hadi kwa Masihi – kikundi cha Al Massira kinaweza kuwa kile unachotafuta.

Jiunge na wengine kwenye ‘safari’ (ya mtandaoni au ana kwa ana) ambapo utakutana na ujumbe wa Biblia usio na kikomo cha wakati: kutazama filamu, na muda wa kujadili na kuuliza swali lolote – na kuona wapi safari hii inakufikisha.

Ikiwa ungependa kujifunza zaidi tafadhali bofya “Jiunge na Kikundi “ hapa chini, jaza fomu ya maswali – na tutakujibu.

Taarifa za Vitendo

  • Kuna vipindi 13 kwa kila takriban dakika 90, na kozi kawaida hufanyika mara moja kwa wiki.
  • Unaweza kufanya Al Massira katika mkutano wa kikundi pamoja ana kwa ana, au unaweza kujiunga na kikundi mtandaoni.
  • Wakati wa kipindi utatazama video fupi chache, kujibu baadhi ya maswali na kupata fursa ya kushirikisha mawazo na mitazamo yako. Kila wiki ina mada tofauti inayoangalia manabii kutokea kwenye maandiko.
  • Video hizo zinapatikana katika lugha nyingi.
  • Vikundi vinaweza kuwa na ukubwa tofauti, kuanzia watu 2 hadi zaidi ya watu 20! Makundi mengine ni ya mchanganyiko, mengine ni wanaume au wanawake tu.
  • Al Massira ni bure, hauhitaji kulipa chochote ili kujiunga.
  • Hakuna ulazima wa kufanya kozi kamili. Unaweza kuanza na kisha ufanye maamuzi ikiwa ungependa kuendelea ili kumalizia.
  • Bofya hapa kujiandikisha kwenye Al Massira.

Ushuhuda