Al Massira -

mahali pa wazi - kutembea na Manabii na kukutana na Masihi

Kozi ya Al Massira inatoa fursa ya kipekee ya kuchunguza hadithi za Mtume na kuzungumza juu ya maswali makubwa yaliyoko katika maisha. Kwa nini ulimwengu uko katika msukosuko? Mungu yuko wapi katika shida zangu na masumbuko yangu? Je, Mungu husikiliza ninapoomba? Tunakualika ujiunge na maelfu ya watu kote ulimwenguni ambao wameanza safari ya Al Massira. Ikiwa ungependa kujiunga katika Kikundi cha Al Massira ili kujenga uzoefu wa safari – tafadhali wasiliana nasi.

Jina la Al Massira linamaanisha “safari”, na lilitengenezwa na kikundi cha marafiki huko Mashariki ya Kati ambao walitaka kuunda ‘mahali pa wazi’ ambapo mawazo yanaweza kushirishwa kwa uaminifu na uhuru, majadiliano yanayofurahishwa kutokana na maswali yanayoulizwa. Ni fursa nzuri ya kupata marafiki wapya, kuchunguza hadithi za nabii na kufikiria kuhusu maswali makubwa ya maisha. Utakutana na watu wengine wanaotafuta ukweli wa kiroho.

five faces AM new-02-02

Taarifa kwa Vitendo

  • Kuna vipindi 13 kwa kila kimoja ni takriban dakika 90, na kozi kawaida hufanyika mara moja kwa wiki.
  • Unaweza kufanya Al Massira kwa kukutana pamoja ana kwa ana kwenye kikundi, au unaweza kujiunga na kikundi mtandaoni.
  • Wakati wa kipindi utatazama video fupi chache, kujibu baadhi ya maswali na kupata fursa ya kushirikisha mawazo na uelewa wako. Kila wiki ina mada tofauti inayoangalia manabii kutokana na maandiko.
  • Video hizo zinapatikana katika lugha nyingi.
  • Vikundi vinaweza kuwa na ukubwa tofauti, kuanzia watu 2 hadi zaidi ya watu 20! Makundi mengine ni ya mchanganyiko, mengine ni wanaume au wanawake tu.
  • Al Massira ni bure, hauitaji kulipa chochote ili kujiunga.
  • Hakuna ulazima wa kufanya kozi nzima. Unaweza kuanza na kisha uamue ikiwa ungependa kuendelea ili kuikamilisha.
  • Bofya hapa kujiandikisha katika Al Massira.

Ushuhuda

"Nimejifunza mengi lakini nilipoanza kuelewa na kuona mambo kutoka kwenye Al Massira ilikuwa ni kama nimeingia kwenye chumba chenye giza na mtu akawasha taa."

Ahmed
kutoka Mashariki ya Kati

"Nilikuwa na maswali kwa miaka ambayo hakuna mtu angeweza kunisaidia kujibu, lakini kupitia Al Massira sasa nimepata majibu ya maswali yangu na amani moyoni mwangu."

Saira
kutoka Mashariki ya Kati

NAMNA YA KUANZA

Jiunge na Kikundi cha Al Massira ili ujifunze kuhusu mpango wa Mungu wa wokovu na kusudi lake kwa maisha yako
Fanya Mafunzo ya Al Massira na ujifunze kushirikisha kwa marafiki zako imani yako kwa Yesu
Al Massira...
1
Lugha

kuathiri watu katika nchi 65 duniani kote

Hadithi Za Hivi Punde

Afrika
Asia
Ulaya
Amerika ya Kusini
Amerika ya Kaskazini

Tuko hapa kusaidia!

Swali lolote tafadhali bofya hapa na tutakujibu.

Video Zetu

Video za Al Massira ni za uhalisia, kwa kutumia fomati za kisasa za media: video zailizochukuliwa mahali husika, vipindi vya kufundisha, mazungumzo, majadiliano ya kuandaliwa, majadiriano ya papo kwa papo, maigizo na shuhuda binafsi.

Kwa nini kuitumia?

Hutoa muhtasari wa wazi wa ujumbe wa Biblia kabla ya kumuhimiza kila mtu afanye uamuzi wake mwenyewe.

jinsi gani unaweza kusaidia

Kuhusu sisi

Al Massira International ni jina la uendeshaji la Al Massira Trust Company Limited kwa Dhamana Namba 08066742 Hisani iliyosajiliwa nchini Uingereza na Wales No 1152547 Reg Office: 2 All Souls Place, London W1B 3DA

Changia

Saidia kazi yetu kwa kutoa mchango kwa PayPal au Stripe